Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud S. Kigahe amefanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam. Ziara hii ambayo imefanyika leo 26/09/2023 ililenga kuangalia changamoto zilizopo pamoja na taratibu za kuzitatua. Aidha, ameweza kuangalia shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kutembelea ujenzi wa jengo la Metrology Annex ambalo litakuwa na ghorofa kumi pindi litakapomalizika.
Jengo hili linatarajiwa kujengwa kwa gharama ya Tshs 22.4 bilioni. Mh. Kigahe amefurahishwa mradi huu ambao unajengwa na kampuni ya Kichina na shughuli inaendelea vizuri. Vilevile ameutaka Uongozi wa Chuo kubiliana na changamoto zilizopo ili kuendelea kutoa elimu bora.